Monday, October 20, 2014

Mchezaji Simba apewa dawa awamalize wenzake


Wachezaji wa Simba wakipeana mawaidha.
Na Mwandishi Wetu
MECHI ya watani haipiti kimya! Simba imefanikiwa kugundua jambo linaloelezwa kuwa kumekuwa na njama zikifanyika kwa ajili ya kuwavunja nguvu wachezaji wake.
Habari za ndani za Simba zimeeleza kumekuwa na njama za kuwawekea madawa yanayoaminika hupunguza nguvu taratibu, hali ambayo imekuwa ikiwafanya wachezaji wake kupoteza nguvu katika kipindi cha pili.
Simba ilianza kufanya uchunguzi baada ya kupata sare ya pili dhidi ya Polisi Moro, uchunguzi huo ulipamba kasi baada ya sare ya tatu dhidi ya Stand United ya Shinyanga na kuna taarifa za kusimamishwa kwa mpishi wake.
Kutokana na hali hiyo, Simba ilianza kuwa makini zaidi na mwisho mmoja wa wachezaji alijitokeza na kueleza kwamba alishawishiwa na viongozi wa timu moja ili achukue dawa na kuweka kwenye chakula ili kuwamaliza nguvu wenzake kwa ahadi ya kupewa mamilioni ya fedha.
Baada ya mchezaji huyo kuamua kujitokeza mwenyewe, baadhi ya viongozi wa Simba waliamua kumuweka kando na kumhoji, naye akaeleza kila hatua ya jambo huku akiwataja baadhi ya viongozi wa moja ya timu kubwa nchini kwamba walimshawishi.
“Kweli jambo hilo limetutisha, linaonekana lilikuwa ni zoezi endelevu maana timu yetu imekuwa ikicheza kipindi cha kwanza tu. Baada ya uthibiti mkubwa, tumeona kweli kuna tofauti, angalia mfano mzuri dhidi ya Yanga, bado timu iliweza kucheza.
“Nakuhakikishia mpishi amesimamishwa, huyu tulimkuta tokea enzi za uongozi uliopita. Sasa viongozi wa Simba wanaendelea na uchunguzi na tukipata ushahidi kwa kweli kuna watu watachukuliwa hatua kali.
“Tumekuwa tukifanya juhudi kubwa kuisaidia timu, halafu kuna watu wanataka kutuumiza makusudi, hili halitakubalika na hakuna kiongozi wa Simba au Friends of Simba atakubaliana na hili,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Viongozi wa Simba walikuwa wagumu kulizungumzia suala hilo kwa madai bado wanafanya uchunguzi.
Mmoja alisema: “Kweli kuna mchezaji kasema, hivyo mtuache kwanza tulifanyie kazi, kwanza tusingependa litoke kwenye vyombo vya habari, mnatuharibia uchunguzi. Itakuwa vizuri mkiacha tukamilishe uchunguzi, halafu tutawaeleza.”
Wakati Simba wanahofia hujuma za madawa yanayopunguza nguvu, watani wao Yanga, juzi waligoma kuingia kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo na kukiteka cha waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Yanga waligoma wakidai walihofia huenda kuna dawa za kuwapunguza nguvu zilikuwa zimepuliziwa katika vyumba hivyo. Hali hiyo ilisababisha waandishi kushindwa kufanya kazi zao.
Kwa upande wa Simba, imecheza mechi nne za Ligi Kuu Bara na kutoa sare zote, hivyo kuifanya iwe na pointi nne tu na kuifanya iwe  na mwendo wa kusuasua.Chanzo:www.globalpublishers.info

HILI NDILO TAMKO LA CHADEMA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA

MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CHA396300_216970381724652_100002350745009_483378_1721045790_nMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA NA KURA YA MAONI KUHUSU KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Dar es Salaam, Oktoba 16, 2014
UTANGULIZI
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imekutana katika kikao chake cha kawaida na kujadili, pamoja na mambo mengine, mchakato wa Katiba Mpya. Kamati Kuu imepata taarifa ya kina juu ya mchakato ulivyoendeshwa katika hatua mbali mbali wakati wa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na marekebisho yake na, baadaye, Sheria ya Kura ya Maoni.
 Aidha, Kamati Kuu imepata taarifa ya mchakato ulivyokuwa katika hatua ya kuundwa kwa Tume ya Mabadiliko, kukusanya maoni ya wananchi na kuandaliwa kwa Rasimu ya Kwanza na ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vile vile, Kamati Kuu imepata na kujadili taarifa ya kina juu ya mchakato wa Katiba katika hatua ya uteuzi wa Bunge Maalum na baadaye ndani ya Bunge hilo. Mwisho Kamati Kuu imepata uchambuzi wa kina wa Katiba Inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalum tarehe 2 Oktoba, 2014.
Uchambuzi huo utatolewa kwa vyombo vyote vya habari na kwa wananchi wa Tanzania kama taarifa hapo baadae.
Baada ya mjadala mrefu na wa kina, Kamati Kuu imeridhika kwamba mchakato wa Katiba katika hatua zake zote ulitawaliwa na nia mbaya iliyokuwa na lengo kuu la kuhakikisha kwamba hakuna mabadiliko yoyote ya maana yatakayofanyika kwenye mfumo wa kikatiba na kiutawala ambao umekuwepo katika nchi yetu kwa zaidi ya miaka hamsini.
 • Mchakato wa kutunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ulitawaliwa na ubabe na usiri uliohakikisha kwamba mchakato wa Katiba unadhibitiwa na Serikali na Chama cha Mapinduzi;
 • Uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum kutoka ‘Kundi la 201’ ulifanywa na Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuhakikisha wajumbe wengi zaidi wa Kundi hilo wanatoka CCM na washirika wake. Kwa sababu hiyo, zaidi ya asilimia 82 ya wajumbe wa Bunge Maalum kutoka Kundi la 201 walikuwa wanachama wa CCM waliochomekwa katika makundi na taasisi mbali mbali;
 • Sambamba na idadi hiyo ya wajumbe wa Kundi la 201, asilimia 72 ya wajumbe wa Bunge Maalum waliotokana na Kundi la Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar walikuwa wanachama wa CCM;
Katika hatua ya mjadala ndani ya Bunge Maalum, Kamati Kuu imeridhika kwamba mjadala huo ulitawaliwa na ukiukwaji wa wazi wazi wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Kudumu za Bunge Maalum.
 • Bunge Maalum lilijigeuza ‘Tume’ na kuanza kukusanya upya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya, wakati kazi ilikwisha kufanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba;
 • Muda wa kuwasilisha taarifa za Kamati mbali mbali ulifupishwa kutoka dakika sitini hadi dakika ishirini na ule wa kuwasilisha maoni tofauti ulifupishwa kutoka dakika thelathini hadi dakika kumi;
 • Utaratibu wa kupiga kura juu ya Katiba Inayopendekezwa kwa njia ya kifungu kwa kifungu uliondolewa na badala yake kura zilipigwa kwa ujumla ya Sura za Rasimu, yaani kura zilipigwa kwa Sura kumi za mwanzo na baadae kwa Sura tisa mwisho;
 • Wajumbe waliokuwa nje ya Ukumbi wa Bunge, au nje ya Dodoma na hata waliokuwa nje ya nchi kwa sababu mbali mbali kama vile mahujaji na wagonjwa waliruhusiwa kupiga kura ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa;
 • Kura za wajumbe waliopinga baadhi ya vifungu vya Katiba Inayopendekezwa na kukubali vifungu vingine zilihesabiwa kuwa kura za kukubali Katiba Inayopendekezwa;
Katika mazingira haya, mambo ya ajabu na yenye kuifedhehesha nchi yetu yaliyotokea ndani ya Bunge Maalum yasingeacha kutokea.
 • Wajumbe Waislamu waliokwenda Makkah kuhiji na ambao uongozi wa Bunge Maalum ulieleza mwanzoni kwamba wangepiga kura kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia hawakupiga kura Ubalozini na haijulikani walipigia wapi kura zao. Aidha, sasa inajulikana kwamba Mahujaji hao – kama ni kweli walifanya hivyo – walipiga kura siku moja kabla ya siku rasmi ya upigaji kura kwenye Bunge Maalum;
 • Licha ya Waheshimiwa Mohamed Raza na Salim Turky – wote wa kutoka Zanzibar – kuharibu kura zao, kura hizo zilizoharibika zilihesabiwa kuwa kura halali za ‘Ndiyo’;
 • Kura za wajumbe waliokufa kama vile Marehemu Shida Salum zilihesabiwa kuwa kura halali za ‘Ndiyo’;
 • ‘Kura za Maruhani’, yaani wajumbe wa UKAWA kutoka Zanzibar na za Wazanzibari wengine waliojitoa na ambao hawajulikani majina yao hadi sasa zilihesabiwa kuwa kura halali za ‘Ndiyo’;
 • Mheshimiwa Maulida Komu wa UKAWA ambaye alitajwa kwenye Gazeti la Serikali lililotangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum kuwa anatoka Zanzibar aligeuzwa na kuhesabika kuwa anatoka Tanzania Bara, wakati Mheshimiwa Zakia Meghji wa CCM aliyetangazwa kwenye Gazeti la Serikali kuwa anatokea Tanzania Bara alihesabika kuwa anatoka Zanzibar na hivyo kupiga kura ya ‘Ndiyo’ kama Mzanzibari;
 • Kura za partly ‘Hapana’ na partly ‘Ndiyo’ zilizopigwa na wajumbe wanne wa kutoka Zanzibar zilihesabika kuwa ni kura za ‘Ndiyo.’
Kamati Kuu imeridhika kwamba, katika mazingira haya, theluthi mbili ya kura za Zanzibar isingeacha kupatikana. Katika mazingira haya, na kwa kipimo chochote, Kamati Kuu imeridhika kwamba upigaji kura ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa ulikuwa batili – na matokeo ya upigaji kura huo – yaani Katiba inayopendekezwa haiwezi kuwa halali.
Na katika mazingira haya, ujasiri unaostahili kupongezwa wa Mwanasheria wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, na wajumbe wengine nane wa Zanzibar waliopiga kura ya wazi ya ‘Hapana’ kuikataa Katiba Inayopendekezwa licha ya shinikizo kubwa, matusi na vitisho vya kila aina, usingeweza kuzuia uharamia huu wa CCM.
Kwa hali hii, Kamati Kuu inaungana na vyama vingine vya siasa vya UKAWA, taasisi kuu za kidini nchini kama vile Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Baraza la Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Shura ya Maimamu, Baraza Kuu la Taasisi za Kiislamu, n.k. kulaani matukio yote yaliyotokea wakati wa mchakato wa Katiba katika hatua zake zote hadi sasa. Kamati Kuu inapondeza na kuunga mkono taasisi, mashirika na vyama vya siasa pamoja na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba waliosusia tukio la Rais Kikwete kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa siku ya tarehe 8 Oktoba, 2014.
Aidha, Kamati Kuu inatoa rai kwa taasisi na mashirika yasiyokuwa ya kiraia ambayo tayari yameshaonyesha msimamo wa kuiunga mkono Katiba Inayopendekezwa kujifikiria upya na kujiridhisha kama mashirika yao hayatumiki kuhalalisha mambo haramu ambayo yamefanywa na CCM na washirika wao katika mchakato huu.
Kamati Kuu imeazimia kwamba CHADEMA itaungana na vyama na taasisi zilizotajwa hapa pamoja na umma wa Watanzania wenye nia njema na taifa kuhakikisha kwamba wanashiriki katika kampeni kubwa na ya nchini ili kuhakikisha kwamba Katiba Inayopendekezwa inapigiwa kura ya ‘Hapana’ katika kura ya maoni, ambayo ni hatua ya mwisho ya mchakato wa Katiba.
Katika hili, Kamati Kuu inatoa rai kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhakikisha kwamba inatekeleza ahadi yake kwa Watanzania kwamba Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litaboreshwa kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni ili kuhakikisha kwamba kila Mtanzania mwenye haki ya kupiga kura anajiandikisha kwenye Daftari hilo na anapata haki ya kushiriki katika maamuzi ya jambo hili muhimu kwa taifa letu.
Kamati Kuu inawakumbusha Watanzania kujiandaa kutimiza wajibu wao wa kihistoria wa kukataa uchakachuaji wa maoni yao uliofanywa na CCM na washirika wake katika Bunge Maalum. Kukataa uchakachuaji huu kitakuwa ni kitendo cha kizalendo cha kila Mtanzania. Kunyamazia au kuunga mkono uchakachuaji huu itakuwa ni kuisaliti nchi yetu na kuendeleza utawala wa kikandamizaji na wa kifisadi ambao umekuwa janga la taifa letu kwa miaka mingi.
——————————————————-
Dr. Willibrod P. Slaa
KATIBU MKUU

MANGULA, NAPE WAONGOZA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akihutubia Jumuia ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu katika Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, lililoandaliwa na Vijana wa CCM wa Vyuo Vikuu, kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo, Oktoba 19, 2014.
Katibu wa NEC, Irikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Mzee Mangula baada ya kuhutubia katika kongamano hilo. Kulia ni Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM mkoa wa Vyuo Vikuu, Christopher Ngubiagai
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika Kongangamano hilo la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Nape amewataka wasomi kutofumbia macho matatizo ndani ya CCM, badala yake wakati wakisifu  mema wawe mstari wa mbele kuyafichua na kuyakemea mapungufu ili chama kiende na wakati
Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM mkoa wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Christopher Ngubiagai akizungumza wakati wa kongamano hilo la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Mwenyekiti wa CCM tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,, Theodora Malata akizungumza mwanzoni mwa kongamano hilo
Washiriki wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kongamano
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba akizingumza kwenye kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa na viongozi wengine meza kuu baada ya kuwasili ukumbini.(Picha na Bashir Nkoromo)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA SHEREHE YA KUWEKWA WAKHFU ASKOFU MTEULE WA KANISA LA AFRICAN INLAND DAYOSISI YA MWANZA, MCHUNGAJI JOHN BUNANGO, JIJINI MWANZA.

1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana nabaadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, Oktoba 19, 2014, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, iliyofanyika jijini humo leo mchana.Picha na OMR2Maaskofu wakimwekea mikono ya Baraka Askofu mwenzao, Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, wakati akiwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, Oktoba 19, 2014. Picha na OMR3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristu, waliohudhuria katika Sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo Oktoba 19, 4Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya kuwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Oktoba 19, 2014. Picha na OMR5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu na wanafamilia ya Askofu  Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya sherehe za kuwekwa wakhfu zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, machana. Picha na OMR6Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, wakati akiondoka Askofu huyo kuwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Oktoba 19, 2014. Picha na OMR7Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu wakati akiondoka kwenye uwanja wa CCM Kirumba, baada ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, leo Oktoba 19, 2014. Picha na OMR

Is ‘Raila factor’ reason behind Uhuru’s shelved tour of Nyanza?

By Dennis Onyango


After the meeting between the Office of the President (OP) and the Kisumu County delegation to plan for President Uhuru Kenyatta’s tour of Nyanza region at Harambee House on Monday, varied reasons have emerged for the postponement of the trip.

Kisumu governor Jack Ranguma
Kisumu governor Jack Ranguma

Kisumu MPs, it is understood, asked for more time to make ‘necessary’ arrangements.

Those who attended Monday’s meeting were Kisumu governor Jack Ranguma, MPs Ken Obura (Kisumu Central), Olago Aluoch (Kisumu West), James Nyikal (Seme), and Onyango Oyoo (Muhoroni).

Others were Fred Outa (Nyando), Aduma Owuor (Nyakach) and Kisumu County Woman Rep Rose Nyamunga.

“It was resolved that the trip be rescheduled to facilitate further consultations between the Office of the President and the leadership of the county,” Ranguma said, adding that the visit would “likely be next week”.

But the area MPs have since given opposing reasons for the postponement of the visit, some pointing at behind-the-scenes political intrigues that marred the planned visit.

They attributed the postponement to the need for “more consultations” and that some MPs had complained about “late invitations”.

Some of the legislators, it was claimed, were not comfortable with the timing of the visit, especially when their party leader and former Prime Minister Raila Odinga, was out of the country.

KAMPENI URAIS CCM: Noti zamwagwa Nec Dodoma

Dodoma. Baadhi ya makada wa wa CCM wanaotajwa kuwania urais kupitia chama hicho wanadaiwa kugeuza mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec), kuwa sehemu ya kampeni kwa wajumbe wa mkutano huo wakidaiwa kumwaga fedha usiku kucha.


Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), wakiwa katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa White House mjini Dodoma juzi na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete. Picha na Ikulu 

Gazeti hili lilishuhudia kampeni hizo zikifanywa na wapambe wa wagombea hao nje ya Ukumbi wa Nec uliopo nje ya jengo la White House mjini Dodoma na baadhi ya watu wanaotajwa kuwania nafasi hiyo.

Wapambe hao kwa siku mbili za vikao vya Nec vilivyofanyika mjini hapa kuanzia juzi walionekana wakifika mapema, kusalimia, kujitenga katika makundi madogomadogo na wajumbe wa Nec tofauti na vikao vingine vilivyotangulia.

Harakati hizo hazikuishia katika viwanja hivyo, bali hata nje ambapo mmoja wa makada anayetajwa kuwania nafasi hiyo kutoka Kanda ya Ziwa ameonekana kukutana na makatibu wa CCM katika moja ya hoteli mjini hapa.

“Huyu jamaa amekutana na makatibu wa CCM mara nyingi katika kile kinachoelezwa kuwa ni kusaka wajumbe ili wasijiunge na kambi nyingine,” kilieleza chanzo chetu.

Alipoulizwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema bado hajazipata taarifa hizo na kwamba kama kuna vitendo vya rushwa vinafanyika ni nje ya mazingira hayo.

Alisema katika mazingira kunapofanyika kikao cha Nec, si rahisi kuwapo vitendo hivyo.

“Sasa kama wanapeana barabarani mimi itakuwa ni vigumu sana. Mimi ninashughulikia na mambo ya humu ndani (kikao cha Nec),”alisema na kuongeza:

Joto uchaguzi Serikali za mitaa lapanda

Na Beatrice Moses, Mwananchi


Dar es Salaam. Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imetangaza ongezeko la idadi ya kata, vijiji, mitaa na vitongoji nchini vitakavyotumika kwa ajili ya uchaguzi serikali za mitaa, huku hatua hiyo ikiibua hoja miongoni mwa wanasiasa na wasomi.

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda 

Tayari vyama vya siasa vimeanza kufanya maandalizi ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14, mwaka huu. Wanasiasa na wasomi wametoa maoni yao kuhusu hatua hiyo, wengi wakilalamikia jinsi isivyokidhi mahitaji ya wananchi na wengine wakielezea kuwa imetangazwa wakati huu kuwanufaisha wachache ili wapate madaraka.

Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kalist Luanda alisema Serikali imeongeza idadi hiyo ili kuanzisha maeneo mapya ya kiutawala ambayo yatawawezesha wananchi kupata huduma za kijamii na kiutawala kwa karibu.

Alisema ongezeko hilo limefanywa kwa kuzingatia idadi ya watu kuongezeka kwa kasi na kupanuka kwa maeneo baada ya watu kujisajili, hivyo kata zimeongezwa na kuwa 465, vijiji 628, mitaa 746 na vitongoji 4,257. Kata kwa nchi nzima zimeongezwa kutoka 3,802 mwaka 2009 hadi 3,337, vijiji vimeongezeka kutoka 11,795 hadi 12,423 na mitaa imetoka 2,995 hadi 3,741 kwa upande wa vitongoji imeongezeka kutoka 60,359 hadi 64,616.

Nape

Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye akizungumzia uamuzi huo aliikosoa hatua hiyo akieleza kwamba idadi ya vijiji vilivyoongezwa ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji yaliyopo.

“Kuna malalamiko mengi kuhusu vijiji hata hivi karibuni kwenye ziara huko Iringa tulifikishiwa malalamiko hayo bado hatujapata uhakika wa vigezo vilivyotumika kuongeza idadi ya vijiji hivyo na kwamba kwa kata mimi sina shida,” alisema.

Saturday, October 18, 2014

MAHAKAMA YA KISUTU YAMZUIA DAVIDO KUPERFORM KATIKA TAMASHA LA FIESTA

MAHAKAMA YA KISUTU YAMZUIA DAVIDO KUPERFORM KATIKA TAMASHA LA FIESTA
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam imemzuia msanii kutoka Nigeria, Adedeji Adelek maarufu kama ‘Davido’ kuperform katika tamasha la Fiesta linaloandaliwa na Clouds Fm na Prime Promotion, October 18,2014. 
Amri hiyo imetolewa jana (October 17) na hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu , mheshimiwa D. Kisoka kufuatia maombi ya dharura yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Times Fm Radio na Times Fm Promotion.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion walipeleka maombi ya dharura mahakamani hapo wakiitaka mahakama kumzuia msanii huyo kuperform katika tamasha hilo kwa kuwa licha ya BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) kukataa kutoa kibali cha msanii huyo kwa maelezo kuwa tayari alikuwa ameshachukuliwa kibali cha kuperform nchini November 1 kwenye tamasha lililoandaliwa na Times Fm Radio, Clouds Fm na Prime Times Promotion waliendelea na taratibu zote bila kujali zuio hilo la BASATA.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion waliiomba mahakama kuidhinisha madai yao dhidi ya Clouds Fm, Prime Promotion na mkurugenzi wa kampuni inayomsimamia Davido, HKN Music.
Madai hayo ni pamoja na kulipwa fidia ya gharama na usumbufu waliosababishiwa na walalamikiwa kadiri Mahakama itakavyoona inafaa.
Mahakama imetoa amri kuwa msanii huyo amezuiwa kufanya onesho hilo October 18,2014 hadi pale ufumbuzi wa kesi hiyo utakapopatikana mhakamani hapo.
Awali, Davido alisikika katika matangazo ya Times Fm Radio akieleza kuwa atakuja Tanzania November 1 kwa ajili ya kufanya onesho linaloandaliwa na kituo hicho cha radio lililopewa jina la ‘The Climax’.

SPIKA MAKINDA AWASILI MUSCAT OMAN KWA ZIARA RASMI YA KIBUNGE


Mhe Spika wa Bunge Anne Makinda akiwa na Naibu Spika wa Majlis A'Shura Sheikh Abdullah Al Majaali aliempokea katika uwanja wa ndege wa Muscat International Airport.
Mhe Spika akiwa na wenyeji wake pamoja na sehemu ya ujumbe wake.Wa kwanza kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Mhe Freeman Mbowe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge),Mhe William Lukuvi.Wa kwanza kushoto ni Mhe Ally Saleh Balozi wa Tanzania nchini Oman. Mhe Spika yuko katika ziara rasmi ya kibunge ya siku sita.
Mhe Spika Anne Makinda wakati akipokelewa uwanjani Mara baada ya kuwasili.